Ticker

20/recent/ticker-posts

Fahamu matumizi mapana ya kitambulisho cha taifa NIDA

     FAHAMU MATUMIZI MAPANA YA KITAMBULISHO CHA TAIFA





Ewe Mwananchi, sasa unaweza kutumia Namba yako ya Utambulisho wa Taifa (NIN)/Kitambulisho cha Taifa (NID) kupata huduma nyingi za kijamii, kiuchumi na kiusalama kama vile;


    BOFYA NAMBA KUANGALIA  KWANAMNA GANI UNAWEZA KUTUMIA KATIKA KAZI HUSIKA HAPO 

    CHINI.

  1. Kusajili Laini ya Simu (Sim Card Registration),
  2. Kusajili Namba Maalumu ya Mlipa Kodi (Tin),
  3. Kusajili Biashara/Kampuni – Brela,
  4. Kukata Hati ya Kusafiria ya Kielektroniki (E-Passport),
  5. Kukata Leseni ya Udereva,
  6. Kupata Huduma ya Afya,
  7. Kufungua Akaunti ya Benki,
  8. Kukopesheka Kirahisi kwenye Taasisi za Fedha,
  9. Kujiunga na Elimu Ngazi Mbalimbali,
  10. Kupata Mkopo wa Elimu ya Juu,
  11. Hati Miliki ya Kiwanja, Nyumba n.k,
  12. Kujidhamini na Kudhamini Wengine,
  13. Kitambulisho cha Taifa kutokana na kuwa na Kisilikoni (Cheap) kinaweza Kutumika kama Pochi ya Fedha ya Kielektroniki (E-Wallet) ambako unahifadhi fedha na kufanya malipo kwa kutumia Kitambulisho Chako,
  14. Kitambulisho kinaweza kutumika kama ATM CARD,
  15. Kwenye Maingio ya Malango Kielektroniki (E-Entrace),
  16. Daftari la Mahudhurio la Kielektroniki (Electronic Attendance),
  17. Mwananchi kuondokana na Adha ya Kubeba Utitiri wa Vitambulisho kwani sasa taarifa zote Muhimu za mwananchi zitapatikana katika Mfumo Mkuu wa Utambuzi wa Watu kwa Kutumia NIN/ Kitambulisho cha Taifa,
  18. Kinaweza kutumika kama hati ya Utambuzi wa Utaifa wa wananchi wanaovuka mipaka ndani ya nchi zilizoko katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwingineko.
  19. Vitaimarisha Utendaji Kazi Serikalini kwa Kuwa na Kumbukumbu Sahihi za Watumishi na Malipo ya Stahili zao, hasa wanapostahafu,
  20. Kupata Ruzuku za Pembejeo za Kilimo Kirahisi,
  21. Kujisajili kwenye Chama cha Ushirika (Kwa Wakulima, Wavuvi, Wafugaji Na Makundi Mengine),
  22. Kupata Msaada wa Tasaf Unaotolewa kwa Kaya Masikini,
  23. Kufungua Akaunti za Benki,
  24. Kuomba Ajira pamoja na Huduma Nyingine Nyingi.

TUMIA SASA NIN/NID YAKO KUPATA HUDUMA ZA KIJAMII, KIUCHUMI NA KIUSALAMA KIRAHISI

“NAMBA YAKO UTAMBULISHO WAKO”

Post a Comment

0 Comments