Ticker

20/recent/ticker-posts

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA UDAHILI KWA MWAKA WA MASOMO 2022/2023




BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI (NACTVET) TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU WAOMBAJI WA UDAHILI WA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2022/2023 

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi linapenda kuufahamisha umma kuwa
 Udahili wa wanafunzi kwa Ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa kozi/programu zote zinazotolewa na Vyuo mbalimbali umefunguliwa rasmi kuanzia tarehe 24 Mei, 2022 hadi tarehe 30 Julai, 2022 katika awamu ya kwanza. Wahitimu wote wa Elimu ya Sekondari na Vyuo wenye sifa za kujiunga na kozi za Astashahada na Stashahada, wanashauriwa kufanya maombi yao kwa umakini ili kupata nafasi ya kujiunga kozi/programu wanazozipenda na ambazo wanatimiza vigezo/sifa za kujiunga nazo kwa mwaka wa masomo 2022/2023. Maombi ya kujiunga na kozi/programu mbalimbali yatumwe moja kwa moja kwenye vyuo husika. Aidha, waombaji wa programu za Afya na Sayansi Shirikishi kwa Vyuo vya Serikali na Visivyo vya Serikali - Tanzania Bara, wanapaswa kuwasilisha maombi yao kupitia Udahili wa Pamoja (Central Admission System – CAS) katika tovuti ya NACTVET (www.nacte.go.tz). Wanafunzi waliopangiwa nafasi za masomo katika vyuo mbalimbali vya elimu na mafunzo ya ufundi na Ofisi ya Rais-TAMISEMI wanajulishwa kuwasiliana na wakuu wa vyuo ili kuthibitisha au kupata maelezo ya namna ya kujiunga na vyuo husika. Wanafunzi ambao hawajaridhika na machaguo yao wanashauriwa kuomba moja kwa moja programu/kozi au vyuo wanavyopenda kuanzia tarehe 24 Mei, 2022. Baraza linasisitiza kuwa wanafunzi waliopangiwa nafasi za masomo na Ofisi ya Rais-TAMISEMI wafanye mawasiliano moja kwa moja vyuoni au ORTAMISEMI kwa maelezo zaidi. Masomo yataanza tarehe 18 Oktoba, 2022. Baraza pia, linawashauri waombaji, wazazi na walezi kuhakikisha kuwa wanaomba kwenye Vyuo ambavyo vimeorodheshwa kwenye Kitabu cha Mwongozo wa Udahili kwa Mwaka wa Masomo 2022/2023 (Admission Guidebook for 2022/2023 Academic Year). Mwongozo wa Udahili unapatikana katika tovuti ya Baraza (www.nacte.go.tz). 

Post a Comment

0 Comments