Ticker

20/recent/ticker-posts

Jinsi ya kupata Leseni ya Biashara online

 



Mfumo wa tausi ni  mfumo ambao upo chini ya Tawala za mikoa na Serikali za mitaa TAMISEMI , mfumo huu umetengenezwa kwa ajili ya mwananchi ambao umekuwa mbadala wa ule mchakato wa awali wa kwenda kwa afisa biashara wa halmashauri husika na kuandikiwa leseni ya biashara kwa mkono kwenye karatasi maalum. 


Mfumo umekuja mahususi kurahisisha mchakato wa upataji leseni za biashara ngazi ya halmashauri, kwani mwananchi anaweza kufanya mchakato wa kuomba leseni akiwa mahali popote kwa muda na wakati anao taka yeye kwa kutumia kifaa chake simu au computer.


Lakini kama ilivyo katika masuala mengine mfano katika suala zima la kuendesha gari mtu unaweza fahamu jinsi ya kuendesha gari au usifahamu  kabisa walakini hata ukifahamu huwezi fahamu kumzidi yule anaetumia gari kila siku, Hivyo katika kuutumia mfumo unaweza kuona ni mchakato mgumu sana japo ni rahisi hususani kwa sisi ambao tuna tumia mfumo huu kuwa saidia watu kila leo kwa si kila huyo anaweza kuendesha gari au kuendesha gari vizuri .


Kupata msaada wa kupata leseni ya biashara unaweza wasiliana nasi ukiwa popote pale Tanzania kwani kwa sababu ya kufanya kazi hii mara kwa mara tutakupa vigezo kama inavyo takiwa ili kufanikiwa katika hili, tunapenda kukaa nawewe ilikukufahamisha mengi ambayo ni rasmi.

Tunapatikana jilani na Kanisa kubwa la Anglikana Barabara iendayo Bank Ya NMB Mpanda katavi wasiliana nasi kwa Namba 0756227816 au 0682329852



Post a Comment

0 Comments